BORA NIENDE(17) - KingSoka Media

Breaking

Saturday, 16 December 2017

BORA NIENDE(17)



BORA NIENDE(17)

KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com

ILIPO ISHIA....
JACK nawasili buguruni alipo mdogo wake huyo Melissa

Jack nafika nakutana na mshichana mrembo Sheila.
Namkamata mkono wakati wa salamu nabakia kumng'ang'ania.
Naingia ndani napo Melisa ananieleza vitu nisivyo vielewa yani nabakia njia panda.
Huku akisema wiki hii anataka kumfanyia kitu mtu ampendae.

SONGA NAYO..........

"Kaka utanielewa tu, maana hii siku niliitamani sana ya kukutana na wewe na kukuambia wewe kaka yangu na kukurambulisha kwa mtu niliyotokea kumpenda sasa japo sikuwahi kufikiria kama nitapenda.
Lakini hata kama ananipenda bado sipo tayari kumvulia nguo yangu hii mpaka pale nitakapo funga nae pingu za maisha aniite mke na mimi nimuite mume.
Hapo ndipo nitafanya mapenzi kwa mara ya kwanza"
Aliongea Melisa na kunifanya gafla nibadilike na kufura hasira huku nikiwa natetemeka mpaka kushindwa kuongea na kubaki nikimtizama tu.
Jinsi alivyokuwa akiongea.

"Kweli umenichoka na ni bora ungeniambia mapema nikajua ili nisije au nije sikutegemea kama nakuja kuutesa moyo wangu.
Melisa kweli nilishindwa kuvumilia lakini sasa ndiyo umeniuwa kabisa, sikutaka kukufosi maana upendo haulazimishi lakini pia jithidi uliyempata awe na mapenzi ya dhati maana vijna wengi hawaaminiki sasa wamegeuza mapenzi kama mchezo na hawajui wanacheza na hisia za mtu"
Niliongea huku nikia siamini kunachonitokea , kama kweli Melissa ninae mjua mimi amepata mpenzi na leo au yani mchana wake pakikucha ananitambulisha.
Roho ilikuwa ikiuma sana mpaka najikuta natetemeka na meno yanagongana ya chini na ya juu.

"Hapana kaka usilie basi nakupenda wewe kaka yangu, na nimekuita ili tu uje nikuambie kama nakupenda na nipo tayari kuishi na wewe, hivyo nakuahidi kuanzia sasa nitakuwa na wewe na nitaishi na wewe nakupenda sana.
Na wewe utakuwa ndiye mume
wangu huku upande mwingine ukisimama kaka yangu.
Na sinta kusaliti nakuahidi nikikusaliti kichwa changu chinjia chini au nipe adhabu yoyote uipendayo narudia kukuahidi tena".
Aliongea Melissa na kunifanya nibaki nikishangaa nikiwa siamini maneno anayo yaongea Melisa .

Ili kuamini kama nikweli anachokiongea melisa alinikumbatia kisha kunitizama na kunitamkia.
"Nakupenda na nirazidi kukupenda"
Nilimtazama bila kupata jibu na kuamua kumvuta kifuani kwangu na kuanza kuunyonya mdomo wake uliokuwa mlaini.
Kila jitu nilichokifa Melissa alikua mgeni hata denda akuwa hakifahamu kupiga zaidi tu aliniachia kila kitu nifanye mimi.

Baada ya kumshika melisa kidogo nilimuona ni mtu mwenye joto kali la hisia hivyo ilinibidi nimuache tu maana pale niliingia kama kaka hivyo ningefnya kitu tayari ningemfanya Melisa anatabia mbaya.
Nilivumilia na kuepusha lawama nilimuomba niondoke lakini alikataa na kuniambia yeye ataenda kulala kwa eafiki yake kama naogopa kulala naye na hatimaye aliondoka na mimi nikafunga mlango nikalala.

Asubuhi nilikua wakwanza kumwamsha ili niondoke kuwahi kufungasha vitu vya dukani nilimpatia pesa ya matumizi na kuondoka zangu huku moyoni nikiwa na kila aina ya furaha kwani hiyo ilikuwa ni furaha kubwa sana kumpata Melisa.

"Hello Jackson natumaini ni mzima tena wa afya na naimai unanijua vizuri mimi n nani.
Mimi ndiye Mr David tajiri mwenye pesa zangu na ninauwezo wa kufanya chochote bila hata kushindwa na nauwezo wa kugeuza ukweli kuwa uongo hivyo baada ya kusoma ujumbe huu nitafute kwa faida yako kabla sijakutafuta mimi"
Ni meseji iliyokuwa nimetumiwa na boss wangu aliye nizulumu nyumba na kunifanya niishi nyumba ya kupanga.
"Wewe niache tu uliyo nifanyia yananitosha lakini bado unanisumbua au unaitaka roho yangu sema tu mimi nije uniuwe na siyo kunipiga mikwara kila siku nimekuchoka Mr David"
Nilimjibu kwa kumuandikia meseji kama alivyo tuma yeye na mimi kuendelea na kazi zangu za kuandika bizaa zilizoisha ili niiende duka la jumla kuongeza vitu vilivyo isha.

"Andika haraka haraka leo nafuraha sana dogo hivyo sema na wewe nikuletee zawadi gani yani namaanisha yoyote uipendayo , na leo nikirudi tu wewe leo ni off yako yani uzurure mpaka saa mbili urudi maana leo nipo na furaha sana"
Niliongea huku nikiendelea kutaja vitu vilivyo isha.
Na hatimaye nilianza safari ya kuelekea soko la tandika kukusanya mzigo wa dukani.

Taratibu nikiwa na kipikipiki changu kidogo nakatika mitaa huku nikiwa na fura ya ajabu kuwahi kutokea,
Furaha niliyo kuwa nayo ilinifanya hata matatizo niliyo nayo niyasahau kisa tu nimempata Melissa msichana niliyempenda na kumjali kwa kila hali .
Na kumuona yeye ndiye kila kitu kwangu na kama ningemkosa basi ningejihisi ni mwenye mkosi katika maisha yangu .

"Kipindindi nikiwa na pesa wengi sana walinipenda lakini niliwakwepa ili nimalize ujenzi wa nyumba yangu, na baada ya nyuma kuisha hata miezi sita sijamaliza ijapigwa mnada.
Bora hata pesa zangu ningezitumia kula bata na warembo waliokuwa wakinitaka kupindi kile na mimi kuwakataa.
Leo niingekuwa hivi mimi natembea na pikipiki"
Niliwaza sana wakati nazidi kuvuta mafuta katika pikipiki yangu ya mzigo.

Baada ya kufika Tazara nimeshaanza kuikamata barabara ya Temeke nilishtuka na mlio mkali wa oni uliopigia nyuma ya pikipiki yangu.
"Piiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii"
Honi ilipigwa bila hata kuachiwa zaidi mpigaji aliendelea kuibonyeza na gafla simu ikaita kucheki ni namba ya Mr David.
"Naomba tukutane Temeke kituo cha usalama katika stendi ya daladala.
Sasa hivi nimekuona hapo na mimi ndiyo niliokupigia honi nazani umenielewa kuna kitu nataka kukuambia"
Aliongea baada ya kupokea simu na alipo maliza alikata bila kunipa nafasi ya kuongea mimi.

ITAENDELEA...................

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here