BORA NIENDE(16) - KingSoka Media

Breaking

Saturday, 16 December 2017

BORA NIENDE(16)



BORA NIENDE(16)

KING SOKA
PHONE:+255717758864
DAR ES SALAAM_TZ
PAGE
#STORY_ZA_KING_SOKA
Email address
jacksonsoka@gmail.com

Sehemu ya kumi na sita iliishia pale nilipo pokea simu kwa mtu nisiye mfahamu na kujitambulisha yeye ni boss wangu.
Nilibaki nimebutwaa huku nikimuuliza boss wangu akajibu ndiyo
Tuliishia hapo


SONGA NAYO.................

"Ndiyo mimi ni boss wako.
Inamaa umenisahau boss wako kisa kukufunga na kukufilisi.
Hahahahahaha! Kijana wewe ni mjinga sana na utakufa masikini, na sisi wenye pesa tutaendelea kula raha za dunia mpaka siku ya kufa na wewe kulia masikini mpaka siku ya kufa"
Aliongea boss wangu na kunifanya nibaki mdomo masikio vyote vikiwa vimepatwa na bumbuwazi.
Kwa maneno aliyoyatoa boss wangu huyo aliysnianya mpaka leo nikiwa naishi nyumba za kupanga kitu ambacho sikuwahi kufikiria katika maisha yangu.

Hakuishia hapo tu bado aluzidi kuongea maneno mengi ya kejeli na zarau.
"Jackson kijana mdogo uliyeingia katika matatizo makubwa ambayo utaweza kuyamaliza kirahisi.
Nakusikitia sana mtu kama uliyekuwa na nyumba nzuri gari na mali za kutosha leo umekuwa kama mbwa wa muokota mifupa"
Aliongea boss wangu akizidi kunikejeli kwa maneno yakunitisha tamaa na kejeli ndani yake.

"Uliku boss wangu zamanu lakini sasa wewe ni binadamu kama binadamu wengine, wewe ni tajiri mimi masikini lakini wote tutaenda chini.
Sikupenda yanitokee yalio nikuta lakini yalisha tokea na sasa naanza upya nyumba yangu imeuzwa chanzo wewe kunisingizia mwizi kwa kitu nisicho husika sasa unazani mimi nitakusamehe vipi katika maisha yangu, mimi nakuchukia kwa kurudisha maisha yangu nyuma tu, na siyo kwa kingine.
Sasa mimi ni masikini tu na sijui lini nitajenga lakini lazima nitajenga, hivyo usinikejeli sana ni moja ya msisha niliyo andikiwa na Mungu.
Jela nimekaa gari yangu umechukua ,nyumba umeuza, lakini vyote ni mali yangu halali lakini kwakuwa wewe pesa unazo unafanya uwezavyo.
Na bado ukurizika sasa umeanza kutaka kuitoa roho yangu kabisa wewe usijali nipo tayari kufa kama ikibidi lakini siyo kwa uwezo wako labda uwezo wa Mungu na Mungu akitaka nife"
Nilimjibu kwa hasira mpaka kila aliyekuwa akipita njiani karibu na duka kusimama na kunisikiliza kwa makini huku watu waliokuja dukani nao walibaki kunishangaa.

Boss wangu huyo akuishia hapo bado alinitukana sana katika simu na sikutaka kukata simu ili nifahamu mengi zaidi kuhusu chanzo cha mimi mpaks nyumba yangu iuwezwe kisa kilikuwa nini.
Nilitamani sana kufahamu chanzo lakini alikata simu na kuniacha njia panda nikijiuliza ni kwa nini amenipigia siku na kunisema kihasi hiki uku akinicheka sana mpaka nilipata hasira.

"Kaka leo nina zawadi nzuri nataka kukupa hivyo ningependa uje huku buguruni leo, ikiwezekana hata kulala utala uku kama ukikosa gari ya kurejea nyumbani, mimi nitalala katika kochi na wewe kitandani.
Niahidi basi kama utakuja yani usichelewe maana ni zawadi nzuri sana msishani mwako na utaifurahiya sana naimani"
Mesagi ya Melisa iliingia katika simu yangu na kunifanya nibaki nikishangaa niende buguruni saa tatu tena ikiwezekana tulale nae chumba kimoja je nikimbaka itakuaje.
Nilitulia kimya kwa muda kisha nikakubalina na Melisa kwa kumjibu mesegi yake kama naenda hivyo aondoe shaka.

Mda mfupi badae niliianza safari ya kuelekea buguruni, huku nyumba nikimuacha kijana aliyekuwa ndiye ananisaidia kuuza duka kwani alikua akilala humo humo ndani nilimpsngia chumba cha kuishi kama yeye, na mimi nikaelekea kupanda gari na safari ikianza.
Hatimaye nilifika buguruni sheli na kushuka .
Na kuanza kurudi kama narimudi vingunguti kuelekea nyumbani kwa Melisa.
Niliwasili ikiwa ni tayari majira ya saa nne na dakika hamsini na sita usiku(23:56 usiku)
"Waooooh kaka umefika!
Ujue siamini kama ni wewe kweli"
Alinipokea Melisa.
Kwa kunirukia na kubembea na shingo yangu mpaka wapangaji wenzake waliokuwa bado wapo njee walishangaa kwa jinsi alivyo nirukia kwa furaha.
"Nimefika namshukuru Mungu kidogo nilipotea lakini nimefika ni jambo la kushukuru"
Niliongea mimi baada ya kuwa nimesha wasili nyumbani kwa Melisa na kumkuta njee amekaa na baazi ya wapangaji wenzake.

"Jamani huyu ni kaka yangu anaitwa Jackson.
Anaishi airport karakata.
Kaka huyu ni Mama Abdul, yule Sheila, huyu mama Issa,na huyo Dada Zakia"
Alinitambulisha Melisa kwa wapangaji wenzake aliokuwa nao njee.
"Namshukuru kuwafahamu pia nashukuru kwa kuishi vizuri na Melissa"
Niliongea huku nikiwasalimia kwa kuwashika mkono.
Nilipofika kwa Sheila ilinibidi nigande kwanza kisha nimuangalie usoni maana.
Mtoto alikua ameumbika akaumbika uzuri wa sura upombo mpaka mavasi, tatizo sikuweza kutambua tabia yake tu.

Nilibaki nimeushikilia mkono wa Sheila bila hata kumuachia huku nikiwa namtazama mara mbili kama siamini kwa ninacho kiona kutokana na uzuri wake alio jaaliwa na mwenyezi Mungu.
"We Kaka!"
Nilishuka baada ya kusikia sauti ikisema we Kaka ndipo nastuka kumbe nimekumbatia mkono wa mtu.
"Samahani Dada nilijisahau unajua leo nipo na furaha sana kukurana na Melisa.
Ndiyo maana"
Niliongea mimi kwa aibu sana uku nikiangalia chini.

"Kaka ujue mimi sina zawadi yoyote ninayo taka kukupa zaidi ya hiki ninachotaka kukuambia Kaka yangu.
Kaka nasikitika kukuambia kama naona undugu unaenda kupotea vile"
Aliongea Melisa kwa sauti ya utaratibu misili ya mtu anaetaka kulia.
"Kwa nini! umesema hivyo Melissa kwani tatizo nini?"
Nilimuuliza Melissa
"Kaka mimi nimeona niolewe tu na atakaye niowa nimesha mpata na kaniahidi kila kitu kizuri na maisha mazuri.
Na pia mpaka leo bado ajafanya kitu chochote mwilini mwangu.
Lakini kwa wika hii nataka nifanye kitu juu yake"
Aliongea Melissa huku akiwa anaangalia chini
"Unasemaje Melissa mbona kama sikuelewi vile"
Niliongea kwa ukali nahisi mpaka waliokuwa njee walisikia.

ITAENDELEA...................

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here